Mkurugenzi wa Tume ya Utumishi wa Waalimu (TSC) Bw.
Erasmus Rugarabamu akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI TAMISEMI
Mhe. George B. Simbachawene (Mb) kutoa hotuba ya Ufunguzi wa kikao cha kazi cha
Tume ya Utumishi ya Waalimu (Teachers Service Commission – TSC) katika ukumbi
wa Taifa wa kuhifadhia nyaraka mjini Dodoma. Waliokaa katikati ni Waziri wa
Nchi TAMISEMI, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume TSC Bw. Oliva Mhaiki na kulia
kwake ni Katibu wa Tume ya Walimu (TSC) Bi. Winfrida Rutaindurwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI TAMISEMI Mhe.
George B. Simbachawene (Mb) akitoa hotuba ya Ufunguzi wa kikao cha kazi cha
Tume ya Utumishi ya Waalimu (Teachers Service Commission – TSC) katika ukumbi
wa Taifa wa kuhifadhia nyaraka mjini Dodoma
Bw. Costantine Machoko akiapa mbele ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B. Simbachawene (Mb) kuwa mjumbe wa Bodi ya
Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC) katika ukumbi wa Taifa wa kuhifadhia nyaraka
mjini Dodoma. Waliosimama kulia kwake ni Mkurugenzi wa TSC Bw. Erasmus
Rugarabamu na Katibu wa Tume ya Walimu (TSC) Bi. Winfrida Rutaindurwa.
Bw. Ramadhani Samainda akiapa mbele ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B. Simbachawene (Mb) kuwa mjumbe wa
Bodi ya Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC) katika ukumbi wa Taifa wa kuhifadhia
nyaraka mjini Dodoma. Waliosimama kulia kwake ni Mkurugenzi wa TSC Bw. Erasmus
Rugarabamu na Katibu wa Tume ya Walimu (TSC) Bi. Winfrida Rutaindurwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI TAMISEMI Mhe.
George B. Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya
Utumishi ya Walimu (TSC) na baadhi ya Wakurugenzi wa TSC waliokaa kulia kwake
ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bw. Oliva Mhaiki na kushoto kwake
ni Katibu wa Tume ya TSC Bi. Winfrida Rutaindurwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George
Simbachawene (Mb) ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kufanikisha ufanisi na kuepuka udanganyifu katika utendaji wake.
Mhe.
George B. Simbachawene (Mb) aliyasema hayo katika kikao kazi cha chombo hicho kilichoambatana na kuapishwa
kwa wajumbe wapya wawili katika ukumbi wa Nyaraka za Taifa Dodoma hapo jana ambapo aliwataka watendaji
wa Tume hiyo kufanya kazi kwa uweledi mkubwa
ili kufikia malengo ya Tume na
kukidhi haja ya wananchi kwa ujumla.
Mhe.
Waziri aliongeza kuwa matarajio ya chombo hiki ni kikubwa hivyo watendaji wanatakiwa kutekeleza majukumu yao yakiwemo kuendeleza na kusimamia utumishi wa
walimu, kuajiri kupandisha vyeo na kuchukua
hatua za kinidhamu kwa walimu na
kumshauri waziri mwenye dhamana na
Serikali za mitaa masuala mbalimbali
yanahusiana na Tume hiyo.
“
Katika sheria ya Mwaka 2015 kifungu
namba 5 kimeainisha majukumu ya chombo hiki ,
matarajio ya Serikali na Wananchi ndio yaliyofanya kuanzishwa kwa chombo
hiki na kimepewa dhamana kubwa kustawisha sekta ya elimu na kupaza sauti kwa
niaba ya walimu ” alibainisha Mhe.Simbachawene
Aidha
Mhe. Waziri alieleza kuwa Tume hii ni chombo cha haki ili kufanya kazi kwa
umakini lazima watendaji wawe waadilifu
kuanzia kwenye ngazi ya wilaya ambao
watakaoenda sambamba na mabadiliko ya
sekta ya elimu na kama hawatenda haki
basi chombo hiki kitashindwa kutimiza majukumu yake ambayo yatafanywa na
vyombo vingine rasmi au sio rasmi .
Pia
aliwataka wajumbe na watendaji wote kuwa makini katika mada zote
zinazowasilishwa katika kikao kazi hicho ili kuendeleza uweledi walinao utakaofanikisha utendaji kazi wa Tume hiyo na
kuhakikisha kazi inafanyika bila
udanganyifu na upendeleo wowote .
Kwaupande
wake Costantine Mashoko ambaye ni mjumbe
wa Tume hiyo amehaidi kuwa wajumbe
watashirikiana na sekretarieti , mwenyekiti , katibu wa Tume pamoja
na wadau mbalimbali wa elimu ili
kutekeleza majukumu kwa uweledi na kuhaidi kuteua watendaji waaminifu ngazi ya wilaya watakaotenda kazi kwa haki.



No comments:
Post a Comment